Sunday, July 19, 2015

Unaathiriki vipi simu yako ikiisha betri ?

Wengi wetu tumejipata katika kizungumkuti hiki, ni ushindani wa kila siku kuhakikisha kwamba simu ya mkononi ina moto wa kutosha na tunakerwa kila betri inapopungua nguvu.
Zamani hali ilikuwa tofauti, simu zilitumika kwa mazungumzo tu na ilikuwa rahisi kwa betri kusalia na nguvu kwa muda mrefu.
Huenda simu zilikuwa nzito wakati huo mithili ya matofali lakini ni kweli pia kuwa nguvu za betri yako zilikuwa zinaweza kukumudu kwa siku tatu.
Lakini sasa imekuwa mtihani wakati tunaona watu waking'ang'ana kufikia swichi za umeme ili kuongeza nguvu simu zao.
Taswira huwa za kustaajabisha, wengine wamesimama katika uwanja wa ndege wengine wakichotama vyooni kufikia swichi wakati wa kuchaji simu zao.
null
Hamu hii kubwa inatokana na kuongezeka matumizi ya simu aina ya smartphones zilizo na apps, ambazo hutumia nguvu nyingi za betri za simu.
Katika nchi kama Rwanda, ambako kunashuhudiwa ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, ni muhimu kuweza kuchaji simu hizo.
Mbinu mpya kote duniani zinasaidia watu kuweza kuhifadhi nguvu za betri katika simu zao kwa muda mrefu - jambo ambalo linazidi kuwa muhimu katika dunia ambapo watu wengi wanaathirika na kuwa na wasiwasi kila wanapokuwa mbali na simu zao.
null
Hali inayojulikana kama - Nomophobia,
Utafiti kutoka chuo kikuu cha Missouri unadhihirisha uhusiano huu unaongeza viwango vya msongo wa mawazo na kusababisha matatizo makubwa ya akili.
Pamoja na simu zenyewe, kuna biashara kamili iliyoanzishwa sasa ya kuwa na vifaa vya kuongeza nguvu betri za simu maarufu zinazojulikana kama Power bank, ilimradi tu unakumbuka kuvichaji pia vifaa vyenyewe.

1 comment:

  1. citizen eco drive titanium watch - India
    In this article we will titanium camping cookware start by mentioning the most popular Indian watches on the market, which are available babyliss pro nano titanium straightener for titanium eyeglasses purchase by t fal titanium pan Indian titanium jewelry for piercings

    ReplyDelete