Kampuni ya Samsung imezindua simu yake nyembamba zaidi aina ya smartphone kufikia sasa.
Simu hiyo kwa jina Galaxy A8 ina upana wa milimita 5.9 ikiwa ni
wembamba wa asilimia 85 ikilinganishwa na simu ya Galaxy S6 Edge.
Licha ya wembamba huo waandisi wameweza kuiweka betri pamoja na kamera yenye uwezo wa mega pikseli 16.
Mmoja ya wataalam aliuliza swali la muhimu wa kutengeza simu nyembamba.
Kwa sasa Samsung imetangaza kwamba simu hiyo itauzwa nchini Uchina na Singapore.
''Galaxy A8 haitauzwa nchini Uingereza'' alisema msemaji wake.
Ijapokuwa
itakuwa simu nyembamba zaidi kutoka kwa mojwapo ya kampuni kubwa
,kampuni nyengine za Uchina tayari zimeanza kuuza simu kama hizo.
Wengi
wetu tumejipata katika kizungumkuti hiki, ni ushindani wa kila siku
kuhakikisha kwamba simu ya mkononi ina moto wa kutosha na tunakerwa kila
betri inapopungua nguvu.
Zamani hali ilikuwa tofauti, simu zilitumika kwa mazungumzo tu na ilikuwa rahisi kwa betri kusalia na nguvu kwa muda mrefu.
Huenda
simu zilikuwa nzito wakati huo mithili ya matofali lakini ni kweli pia
kuwa nguvu za betri yako zilikuwa zinaweza kukumudu kwa siku tatu.
Lakini sasa imekuwa mtihani wakati tunaona watu waking'ang'ana kufikia swichi za umeme ili kuongeza nguvu simu zao.
Taswira
huwa za kustaajabisha, wengine wamesimama katika uwanja wa ndege
wengine wakichotama vyooni kufikia swichi wakati wa kuchaji simu zao. Hamu hii kubwa inatokana na
kuongezeka matumizi ya simu aina ya smartphones zilizo na apps, ambazo
hutumia nguvu nyingi za betri za simu.
Katika nchi kama Rwanda, ambako kunashuhudiwa ongezeko la matumizi ya simu za mkononi, ni muhimu kuweza kuchaji simu hizo.
Mbinu
mpya kote duniani zinasaidia watu kuweza kuhifadhi nguvu za betri
katika simu zao kwa muda mrefu - jambo ambalo linazidi kuwa muhimu
katika dunia ambapo watu wengi wanaathirika na kuwa na wasiwasi kila
wanapokuwa mbali na simu zao. Hali inayojulikana kama - Nomophobia,
Utafiti
kutoka chuo kikuu cha Missouri unadhihirisha uhusiano huu unaongeza
viwango vya msongo wa mawazo na kusababisha matatizo makubwa ya akili.
Pamoja
na simu zenyewe, kuna biashara kamili iliyoanzishwa sasa ya kuwa na
vifaa vya kuongeza nguvu betri za simu maarufu zinazojulikana kama Power
bank, ilimradi tu unakumbuka kuvichaji pia vifaa vyenyewe.